Genesis 36:31-43

Watawala Wa Edomu

(1 Nyakati 1:43-54)

31 aWafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:

32Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.
33 bBela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
34 cYobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
35 dHushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
36Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
37 eSamla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake.
38Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
39Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.

40 fHawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao:

Timna, Alva, Yethethi,
41Oholibama, Ela, Pinoni, 42Kenazi, Temani, Mibsari, 43 gMagdieli na Iramu. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki.
Huyu ndiye alikuwa Esau, baba wa Waedomu.

Copyright information for SwhNEN